Would you like to switch language?
From Ajakai ICT Says:

Jobs Membership
Connection Za Kazi

Ndani na Nje ya Nchi

Kwanini Ujiunge?

Ngoja Nikueleze Kitu Hapa!

Kuna wakati unaweza kuwa mbali na michongo ya kazi inayotumwa toka makampuni au taasisi mbalimbali na kwakuwa unaweza kuwa umetingwa na majukumu ya kifamilia au kikazi, au uko sehemu ambayo mtandao ni shida sana kupatikana, au huna marafiki wa kukujulisha michongo ya kazi, au hata huna simu janja.

Basi ondoa shaka Ajakai ICT tumelifahamu hilo, sasa unaweza ukajiunga kwenye mfumo wetu ili tukupe connection mbalimbali za kazi zinazotangazwa au zilizotufikia ofisini. unapokuwa mwanachama wetu tutakutumia maombi mbalimbali na kukuunganisha katika makampuni au taasisi mbalimbali zinazohitaji wafanyakazi. Pia tutakusaidia kuandaa cv na vyeti vyako kwa umahili wa hali ya juu ili ziwe katika kiwango cha juu kwa mwajiri au mpokea maombi. Tuna zaidi ya miaka mitano(5) katika hii kazi na ndiyo maana tumeshatengeneza connection nyingi za ndani na nje ya nchi.

Baadhi ya Nchi Tulizo Na Connection

Tanzania, Congo, Mali, Liberia, Siera Leone, Saud Arabia, Sudan, Somalia, Zambia, Canada, Australia, USA, na zingine nyingi.

Faida za kuwa Mwanachama
  • Tutatoa punguzo la asilimia 20% kwa huduma utakayofanya(kama kurekebisha CV, kupangilia vyeti, kuskan, kuedit, kuprint, nk) .
  • Tutakupatia taarifa za kazi mpya punde zitakapotangazwa.
  • Tutakutumia maombi ikiwa utahitaji popote pale utakapokuwa.
  • Endapo kwa muda husika hutakuwa na pesa za malipo, tunaweza kufanya kazi yako na kisha deni litaandikwa
Tunafanyaje Kazi?

Mwanachama anapojisajiri katika mfumo wetu, nyaraka zako ni lazima ziwe na sifa zifuatazo:

  • Mwanachama anatakiwa awe na CV ya kisasa yenye ushawishi kwa mwajiri:
    Waombaji wengi wa kazi wana CV ambazo zimepangiliwa vibaya na hazina mvuto wowote kwa anayeiptia. Kuna vitu vinatakiwa kuandikwa kwenye CV na kwa kufuata mpangilio mzuri. Utakapofaulu kupangilia vizuri CV yako utaweza kupunguza idadi ya kurasa nyingi zilizoandikwa. CV inapokuwa na kurasa chache isiyozidi kurasa 2 na yenye mvuto, utaweza kumshawishi mwajiri kuipitia CV hiyo na kushawishika.
  • Mwanachama anatakiwa apangilie vyeti vyake vyote vya huduma, mafunzo na taaluma kwa mtiririko mzuri na muonekano:
    Unapotuma vyeti vyako ambavyo havipo kwenye mpangilio na kuweka vyeti ambavyo havihusiani na kazi yako na pia wengine huvipiga picha ambavyo vinakuwa havina ubora au vimekaa upande, hapo ni kujikosesha kazi mwenyewe hata kama una sifa. Mwajiri hawezi kupoteza muda wake kupitia vyeti vyako.
  • Mwanachama anatakiwa kuambatanisha baadhi ya vitambulisho (Kama unavyo):
    Hapa vitambulisho vinavyohitajika ni kama leseni ya udereva, passport ya kusafiri, vitambulisho vya kazi kama work permit na vingine vya muhimu kama unavyo.
Majukwaa Tunayotumia

Tunatumia majukwaa mbalimbali yanayotanganaza nafasi za kazi za ndani na nje ya nchi. Pia tunapata nafasi za kazi ambazo zinatumwa toka kwa wadau wetu waliopo katika makampuni mbalimbali ya ndani na nje endapo wanahitaji wafanyakazi, nafasi hizo zinaweza kutufikia kwakuwa wakijua kuwa kuna wadau wetu wapo katika kampuni husika na wanafanya vizuri.

Majukwaa mengine tunayoyatumia ili kusaidia wanachama wetu kupata kazi kiurahisi ni pamoja na LinkedIn, Glassdoor na Indeed, Tunamsaidia mwanachama kumfungulia akaunti katika majukwaa hayo na kuendesha akaunti yake akihitaji, kwakuwa tunajua wengi siyo wazuri katika matumizi ya mitandao.

Mitandao hiyo inafaida sana utakapojiunga, ngoja nitoe maelezo mafupi kuhusu mtandao wa LinkedIn:
LinkedIn ni mtandao wa kijamii wa kitaalamu unaotumiwa sana na wataalamu na waajiri kuunganisha, kushirikiana na kutafuta fursa za kazi. Hapa kuna mambo muhimu kuhusu LinkedIn:

  • Mtandao wa Kijamii wa Kitaaluma: LinkedIn ni mahali ambapo wataalamu kutoka sekta mbalimbali hukutana, kubadilishana mawazo, na kushirikiana kwenye miradi.
  • Kuweka Wasifu wa Kitaaluma: Watumiaji wanaweza kujaza wasifu wao na taarifa za elimu, ujuzi, uzoefu wa kazi, na mafanikio mengine ili waajiri waweze kuwaona.
  • Kutafuta na Kutangaza Kazi: Makampuni mengi hutumia LinkedIn kutafuta wagombea wa kazi na kutangaza nafasi za kazi. Watumiaji wanaweza kutafuta kazi na kutuma maombi moja kwa moja kupitia mtandao huu.
  • Mafunzo na Kujifunza: LinkedIn inatoa kozi za mafunzo kupitia LinkedIn Learning ambazo zinaweza kusaidia kuboresha ujuzi wa watumiaji.
Usimamizi na uendeshwaji wa akaunti

Utakapojiunga na kifurushi ambacho utatupa ruhusa ya kuendesha akaunti yako, basi tunahakikisha akaunti yako inaonekana vizuri na yenye ushawishi kwa watakayoipitia. Tuta follow au connect na kuchat na watu mbalimbali ambao wenye wadhifa mkubwa katika makapuni mbalimbali ili kuweza kuwa nao karibu, na kuipitia akaunti yako mara kwa mara.

Vifurushi vya kujiunga Uanachama
STARTER PLAN (25,000/Mwaka)

  • Kupewa taarifa juu ya kazi zilizotangazwa ndani na nje ya nchi zilizotufikia
  • Kutumiwa maombi ya kazi kulingana na nafasi yako katika kazi kwa Email
  • Kuandikiwa barua ya ombi la kazi pale inapohitajika
  • Kuwasiliana na watoa huduma wetu, kuulizia mambo yanayohusiana na kazi
AGENCY PLAN (70,000/Mwaka)

  • Kupewa taarifa juu ya kazi zilizotangazwa ndani na nje ya nchi zilizotufikia
  • Kutumiwa maombi ya kazi kulingana na nafasi yako katika kazi kwa Email na Mifumo
  • Kuandikiwa barua ya ombi la kazi pale inapohitajika
  • Kuwasiliana na watoa huduma wetu, kuulizia mambo yanayohusiana na kazi
  • Kutengenezewa au kuboreshewa akaunti ya LinkedIn
ENTERPRISE PLAN (150,000/Mwaka)

  • Kupewa taarifa juu ya kazi zilizotangazwa ndani na nje ya nchi zilizotufikia
  • Kutumiwa maombi ya kazi kulingana na nafasi yako katika kazi kwa Email na Mifumo
  • Kuandikiwa barua ya ombi la kazi pale inapohitajika
  • Kuwasiliana na watoa huduma wetu, kuulizia mambo yanayohusiana na kazi
  • Kutengenezewa akaunti ya LinkedIn, Glassdoor na Indeed na uendeshwaji wa akaunti hizo
  • Kupewa au kutumiwa majibu mbalimbali yaliyorudi katika kazi iliyoombwa
Vigezo na Masharti

Soma maelekezo hayo kwa umakini kabla ya kujiunga kuwa mwanachama, Utakapokiuka maelekezo hayo basi Uwanachama wako utafutwa na pesa zako hazitorudishwa

  • Unapokamilisha kujiunga hakikisha unatuma CV na Vyeti vyako ili viingizwe kwenye akaunti yako ya uanachama na ofisi pia iwe na nyaraka zako kwa kurahisisha kukutumia nafasi ya kazi pale zinapotufikia
  • Utakapokamilisha usajiri na hujalipia gharama ya uanachama Tsh 25,000 ndani ya wiki moja (siku 7) taarifa za akaunti yako itafutwa
  • Kwa kila nafasi ya kazi tutakayokutumia utatozwa nusu gharama ya mteja wa kawaida. Yaani kazi itakayotumwa kwa kutumia email utatozwa Tsh 500 na itakayotumia mfumo yaani kukusajiri kwenye mfumo husika na kutuma ombi lako la kazi ni Tsh 1,500 hadi Tsh 3,000 na gharama hizo zitaandikwa kama deni kwenye akaunti yako
  • Deni lako linatakiwa kulipwa ndani ya siku 28 baada ya kutumiwa ombi lako la kazi, na unaweza ukalipia zaidi ili kupunguza usumbufu huo. na tutakuwa tunakata salio liloongezeka kwa kila kazi tutakayokutumia
  • Unatakiwa kupitia Email yako mara kwa mara ili kujua mrejesho wa ombi lako la kazi tuliyokutumia, Kama huna simu janja basi unatakiwa kutoa taarifa mapema ili tuone namna ya kukusaidia
  • Unatakiwa kupitia mara kwa mara App hii sehemu ya Waliotumiwa nafasi za kazi kwa wanachama au kuingia kwenye akaunti yako ili kujua sehemu ulizotumiwa na deni unalodaiwa
  • Utakapopigiwa simu za nje au ndani ya nchi kuhusu nafasi ya kazi tuliyotuma au kupokea email kwa maelekezo juu ya kazi uliyotumiwa tunaomba ushirikiano wako kutujulisha ili tushirikiane kufaulu Interview au ujazaji wa fomu zao na mahitaji mengine

MSISITIZO:
Kutofuata maelekezo hayo uwanachama wako unaweza ukafutwa. Toa taarifa mapema endapo kama unachangamoto yeyote. Tuwe Serious na wavumilivu tunapohitaji vitu Vizuri