Would you like to switch language?
From Ajakai ICT Says:

News Details
Ufanye nini endapo Kompyuta yako haiwaki kabisa?
Tech Tutorials Hardware Setup

Wakati mwingine Kompyuta zetu huwa zinawaka lakini hakuna kitu kinachoonekana kwenye kioo, Hupati kiashiria chochote kuwa imewaka kioo ni nyeusi tu. au huweza ona taarifa kwenye kioo kuwa "No VGA cable" au "Check the Video cable" error. Kwa tatizo hilo kuna vitu vingi huweza kusababisha, Na ili iweze kuwaka kama kawaida itabidi utatue/urekebishe baadhi ya vitu katika kompyuta yako,

Twende pamoja kwa hilo somo ili kutatua tatizo lako, ili kompyuta yako irudi katika hali ya kawaida




Sawa hapo Swali ni kipi kulichosababisha mpaka Kompyuta yako isiwake? na jinsi gani ya kuweza kutatua hilo tatizo? Jibu litapatikana ni baada ya kufanya hatua zifuatazo moja baada ya nyuingine:



HATUA YA KWANZA:

Angalia kioo (Monita) yako Vizuri; Kitu cha kwanza inabidi ujidhihirishe kuwa je Monita yako inapata umeme na inawaka? Siyo hivyo tu bali je waya wa data (VGA cable) imechomekwa vizuri? Huwaenda pini zake zimekatika au kupinda.



HATUA YA PILI:

Angalia kadi ya picha (Graphic Video Card); Fungua ndani ya kompyuta yako na uhakikishe kadi ya picha imechomekwa vizuri kwenye saketi (Motherboard). Jaribu kuitoa hiyo kadi Safisha vumbi alafu irudishie tena kwa kuiweka sahihi, na uwashe tena kompyuta yako, ili kujua kuwa huenda tatizo likawa hilo. Kama kompyuta yako imewaka basi ulikuwa na tatizo la Kadi ya picha.


HATUA YA TATU:

Angalia Vifaa vingine ndani ya kompyuta: Wakati mwingine baadhi ya vifaa (Hardware) kama havijachomekwa vizuri kama HDD,CD ROM yaweza sababisha tatizo hilo, hakikisha unachomoa vyote na kuchomeka tena upya, kisha washa tena kompyuta yako.

HATUA YA NNE:

Angalia CMOS Battery; Wakati mwingine CMOS battery linapochoka au kukaa vibaya huwa linasababisha tatizo lingine kama la kutokuwa kompyuta na hata lingine zaidi, hivyo basi jaribu kulitoa pia na uliweke tena vizuri na uwashe tena kompyuta yako, kama tatizo siyo hilo tuendele na hatua nyingine




HATUA YA TANO:

Angalia RAM; Kuna asilimi 90 ya tatizo la RAM husababisha kompyuta kuto kuwaka, kwakuwa hapo ndipo sehemu muhimu sana ni kama njia ya kutoka kwenye ubongo na kutuma taarifa sehemu zingine. Endapo kama RAM imekufa Kompyuta haiwezi kutoa picha kwenye kioo (Monita) na hata sakiti (Motherboard) wakati mwingine haitowaka. Sasa kama una RAM mbili kwenye kompyuta yako jaribu kutoa moja na uache moja kisha washa kompyuta yako, kama bado jaribu uliyotoa au weka kwenye shimo (slot) nyingine huenda RAM moja au Shimo (slot) moja imekufa. Pia hakikisha unapotoa hizo RAM una zisafisha vizuri makalio yake, kama hujui jinsi ya kusafisha tafadhari andika Comment mwisho wa post hii ili nikuelekeze, maana hapo unahitaji kuhakikisha kuwa kila kitu kipo sawa ndipo twende hatua inayofuata.






HATUA YA SITA:

Angalia Ubongo wa Kompyuta (CPU); Hii ni hatua ya mwisho baada ya kushindikana kwa vyote, kwa kuwa ubongo wa kompyuta ni mara chache sana kuharibika, ni kama asilimia 1 tu ya tatizo la ubongo (CPU), Jaribu kutoa ubongo Safisha vizuri na uweke tena, huenda labda umekaa vibaya. Kisha washa tena kompyuta yako.



Kama hujaweza kufanikiwa kwa hizo hatua zote Comment ili niweze kukusaidia zaidi. Asante

HTML Comment Box is loading comments...
Share to