Huu hapa ni muongozo wa hatua kwa hatua utakazopitia unapoomba kazi katika nchi nyingine za Afrika, ukiwa bado ndani ya bara la Afrika:
Chagua nchi unayopendelea (mfano: Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Kenya, DRC, Zambia, n.k.)
Fanya utafiti kuhusu sekta zinazohitaji wafanyakazi (mfano: madini, ujenzi, afya, elimu, IT, n.k.)
Andika CV ya kimataifa (inayoeleweka Afrika Mashariki, Kusini au Magharibi)
Hakikisha CV ina:
Maelezo ya mawasiliano (email, simu, WhatsApp)
Uzoefu wa kazi (nafasi, kampuni, muda, majukumu)
Elimu, ujuzi na vyeti vya kitaaluma
Eleza kwa nini unaomba kazi katika nchi husika
Onyesha ujuzi wako, uzoefu na utayari wa kufanya kazi nje ya nchi yako
Tumia tovuti zinazotoa kazi Afrika kama:
Tafuta kazi zenye kichwa:
"Expat Jobs"
"Foreign Workers"
"East/Southern/West Africa Jobs"
Tuma CV + barua ya maombi kwa waajiri wa moja kwa moja au kupitia makampuni ya uajiri
Hakikisha unaweka njia rahisi za kuwasiliana: simu, barua pepe, WhatsApp
Tumia LinkedIn kuwasiliana moja kwa moja na HR au meneja wa kampuni
Waajiri wengi hufanya mahojiano kwa njia ya Zoom, Skype au simu
Jiandae kuulizwa kuhusu uzoefu wako, kwa nini unataka kuhamia, na uwezo wako wa kuendana na tamaduni mpya
Ukifaulu, utapewa barua rasmi ya kazi ikieleza mshahara, nafasi, muda wa mkataba na masharti mengine
Baadhi ya waajiri hushughulikia vibali vya kazi (Work Permit) kwa niaba yako
Nchi nyingi za Afrika huhitaji work visa au residence permit
Wasilisha barua ya kazi, pasipoti, picha, vyeti, na nyaraka nyingine kwenye ubalozi au online
Kwa nchi jirani, unaweza kupewa visa mpakani lakini hakikisha unafuata sheria rasmi
Ukikubaliwa visa au kibali cha kazi:
Nunua tiketi ya ndege au basi (inategemea umbali)
Kuna baadhi ya makampuni huwa tiketi ya ndege wanaandaa wenyewe na kukutumia ili kuanza safari
Andaa makazi ya muda au unaweza ukafikia camp ya kampuni
Tafuta msaada kwa wana diaspora au jamii ya Watanzania/Waafrika nchini humo
Wasiliana na mwajiri
Fanya usajili wa ndani kama inavyohitajika (kodi, leseni ya kazi, bima ya afya)
Fuata taratibu zote za nchi husika ili kuepuka matatizo ya uhamiaji
Usitumie mawakala wasioaminika – fuatilia mwenyewe au tumia tovuti rasmi
Angalia viza zinazopatikana kwa urahisi (mfano: Zambia, Rwanda, Kenya, Ghana n.k.)
Jifunze misingi ya lugha ya nchi unayolenga (mfano: Kifaransa, Kireno au Kiarabu)
Jiunge na makundi ya Facebook/WhatsApp ya Africans Working in [Country]
Utakapotuma ombi la kazi, usikubali kutuma pesa yeyote kabla ya kufanya mahaojiano (interview) na kutumiwa ofa ya kazi katika kampuni husika.
Jiunge nasi ili tukusaidie kukupa connection za kazi na msaada wa kuandika CV ya Afrika kwa nafasi unayolenga